UNAMJUA RAIS WA MASHABIKI WA MTIBWA SUGAR DUNIANI?

Shabiki mkubwa wa Mtibwa Sugar Suleiman Nassoro ‘Super Cicinho’ amesafiri kutoka visiwani Zanzibar hadi Dar ili kuishuhudia timu yake wakati ikicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Yanga siku ya Jumamosi August 6 kwenye uwanja wa taifa.
Rais wa Mashabiki wa Mtibwa Sugar yenye maskani yake Turiani Mkoani Morogoro Suleiman Nassoro ‘Super Cicinho’ ambaye alipata umaarufu sana katika Mashindano ya kombe la Mapinduzi mwaka huu, leo asubuhi mapema ameelekea jijini Dar es Salam kuiunga mkono timu yake ambapo kesho wanacheza mchezo wa kirafiki na Yanga.
Mtandao huu ulimnasa rais huyo akiwa Bandarini, Malindi mjini Unguja akielekea kupanda boti na tukataka kujua anakwenda wapi ndipo akafunguka kama yeye ndiye rais wa mashabiki wote wa Mtibwa anakwenda Dar es Salam leo ili kesho aione timu yake ikicheza na Yanga.
“Nakwenda Dar kuingalia timu yangu Mtibwa kesho tunacheza na Yanga, mimi lazima niende huko kwasababu hivi karibuni niliteuliwa kuwa rais wa mashabiki wote wa Mtibwa sasa lazima nikaangalie chama langu, nadhani watu wananijua mimi na kaka yangu kuwa tunapeperusha bendera ya Mtibwa Zanzibar na ndio mana mwenye timu akanipa cheo cha kuwa Rais wa Mtibwa maana kombe la Mapinduzi limenipa umaarufu sana hasa kupitia mtandao wa Shafih Dauda waliponirusha,” alisema.
Suleiman Nassoro ‘Super Cicinho’ amepata umaarufu sana yeye na kaka yake maarufu kama Saleh Miwa baada ya kuwa mashabiki wakubwa wa Mtibwa Sugar Visiwani Zanzibar.
Saleh Miwa kaka wa Suleiman Nassoro ‘Super Cicinho’ nae pia ni shabiki mkubwa wa Mtibwa Sugar.



Source:Shaffihdauda.com

































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..