Wapewa siku sita majina ya watumishi hewa..
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki.
Taasisi za umma 145 zimetakiwa kuwasilisha orodha ya watumishi hewa kabla hayajamkabidhi kwa Rais John Magufuli.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki ametoa siku sita kwa taasisi hizo ili taarifa ya mwisho ikabidhiwe kwa Rais kwa hatua zaidi.
“Taasisi 63, waajiri wake wamethibitisha hawana watumishi hewa na nyingine 201 zimeleta taarifa za kuwapo watumishi hao kuanzia mmoja na kuendelea,” amesema Kairuki.
Maoni
Chapisha Maoni