AGUERO NA NOLITO WAPIGA MBILI-MBILI CITY IKIITWANGA STOCK CITY BRITANIA..
Manchester City chini ya Guardiola wakiwa ugenini wameendeleza wimbi lao la ushindi baada ya kuifumua Stock City mabao 4-1.
Sergio Aguero na Nolito kila mmoja amefunga magoli mawili na kuipa City ushindi huo mnono na kuendelea kupambana kileleni na mahasimu wao Manchester United.
Goli la Stock City lilifungwa na Bojan Krkic.
Kauli za makocha baada ya mchezo
Bosi wa Stoke City Mark Hughes amesema: “Penati zilikuwa muhimu, hasa ile moja ambayo ilikuwa dhidi yetu kwenye kipindi cha kwanza. Kuna mabadiliko makubwa sana ya sheria kwenye msimu huu wa ligi. Ilitutoa mchezoni kabisa.
“Penati yetu pengine kama ingekuwa msimu uliopita isingetolewa, lakini ilitusaidia kurudi mchezoni mpaka tulipofungwa goli la tatu na kutoka kabisa mchezoni kabisa. Lakini siamini kama matokeo haya yameakisi mchezo ulivyokuwa.
“Kiukweli kwa mwaka huu Man City ni klabu kubwa hasa, na hatukuweza kupambana nao kutokana na kasi waliyokuwa nayo.”
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema: “Nafahamu vizuri namna gani wachezaji walivyo na ubora, najisikia ni mwenye bahati kubwa kutokana na ubora wa wachezaji niliokuwa nao hapa.
“Wanacheza mpira kwa kasi, wanakaba, na leo tumecheza katika moja ya viwanja vigumu sana kwenye ligi hii. Imenisikitisha kidogo kwamba tumetengeneza nafasi nyingi kipindi cha pili lakini hatukuweza kumalizia vizuri.
Source:Shaffihdauda.com
Maoni
Chapisha Maoni