Samaki wasababisha vifo vya watu wawili..
Samaki wanaodaiwa kuvuliwa kwa sumu wamesababisha vifo vya watu wawili ambao wamechomwa moto.
Watu hao walipigwa kisha miili yao kuchomwa moto na wananchi katika Kijiji cha Nyamelele, Kata ya Nkome baada ya kubainika kuwa wamebeba samaki waliokuwa wamevuliwa kwa sumu kwenye pikipiki zao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo lilitokea juzi Saa 11:00 alfajiri na alimtaja mmoja kuwa ni Franco na mwingine maarufu kwa jina la Pere.
Source:Mwananchi
Maoni
Chapisha Maoni