African Boy ya Jux yaingia kwenye urembo wa simu..

Msanii wa muziki wa R&B Jux baada ya kufanya vizuri na biashara ya t-shirt, sneakers pamoja na mabegi ya brand yake ya African Boy, Jumatano hii ametangaza bidhaa yake mpya.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Wivu’, ameshare kwa mashabiki wake picha ya kava za simu zenye logo ya African Boy.
“AfricanBoy covers now available at Starlook. Follow Fatma8five for more details. These joints are so swaggy though,” aliandika Jux kwenye instagram.
Jux amekuwa akikaririwa na vyombo vya habari akisema kwamba, biashara ya nguo kupitia brand yake ya African Boy ni moja kati ya vitu vinavyomwingizia pesa ngingi.



Source:Bongo 5











































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..