TCRA imeanza mpango wa ugawaji wa masafa ya mawasiliano kwa njia ya mnada.

Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA kwa mara ya kwanza imeanza mpango wa ugawaji wamasafa ya mawasiliano kwa njia ya mnada ili kuleta ushindani kwa kampuni zinazotoa huduma ya mawasiliano kwa jamii ili yawe bora kitechnologia na yenye wigo mpana kwa wananchi wote wa mijini na vijijini.
Akizungumzia mpango huo jijini Dar es Salaam katika mkutano uliowakutananisha wadau wa mawasiliano na mamlaka ya mawasialiano nchini mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Profesa John Nkoma amesema kuwa TCRA imeamua kufanya hivyo kutokana na ushindani mkubwa uliopo wa makampuni ya mawasiliano nchini yanayopelekea masafa kuwa machache ukilinganisha na makampuni yaliyopo jambo ambalo limelazimu uwepo wa uwazi katika ugawaji wa masafa hayo ili kuwa chanzo cha kuliongezea taifa pato.
 
Kwa upande wake mhandisi wa masafa kutoka TCRA Bwana Victor Kweka ameeleza kuwa licha ya kuwa mfumo huo wa ugawaji wa masafa kwa njia ya mnada ni kwa mara ya kwanza nchini lakini utasaidia sana wananchi wa vijijini kufikiwa na mawasiliano kutokana na masafa ya technologia mpya kuhitaji minara michache kwa wigo mpana wa mawasiliano.
 
Mpango huo unatarajiwa kuanza kutumika October mwakani baada ya wadau wote wa mawasiliano kushirikishwa ambapo kampuni ambazo zitashinda kwa kufikia vigezo vitakavyowekwa katika mnada utakaotangazwa ndizo zitakazo gawiwa masafa.
Source(ITV)
 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..