Wagonjwa wanahudumiwa katika kituo cha Afya Kaigara hatarini kukumbwa na mlipuko wa Magonjwa
Wagonjwa wanahudumiwa katika kituo cha afya cha Kaigara kilichopo wilayani Muleba mkoania Kagera wapo hatarini kukumbwa na mlipuko wa magonjwa kutokana na kukosekana kwa huduma ya maji katikta kituo hicho kwa zaidi ya miezi sita.
ITV imeshuhudia baadhi ya akinamama wajawazito na watoto waliotoka katika kituo hicho cha afya cha kaigara wakichota maji katika mto uliopo umbali mbali kidogo na kituo cha afya Kaigara ambapo wameileza ITV adhaa kubwa wanayo ipata kutokana kukosekana kwa huduma ya maji katika kituo hicho.
Hali hiyo imejitokeza mara baada ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Muleba kubaini tatizo hilo huku wakiitupia lawama serikali kushindwa kuweka huduma ya maji pamoja na jenereta ya dharuara kwaajili ya kusabambaza umeme na maji katika kituo chicho cha Afaya Kagigara ambacho nitegemeo la wakazi wa wilaya nzima ya muleba huku wakieeleza kusikitishwa na kitendo cha kukosekana kwa huduma muhimu ya maji katika kituo hicho.
Kwa upande wake mganga mkuu wa wilaya ya Muleba Dk. Leontine Lwamulaza amekiri kuwepo kwa ukosefu wa huduma ya maji na amesema tatizo hilo limejitokeza mara baada ya mashine ya kupampu maji kuharibika.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Muleba Joseph Mkude amesema tatizo hilo limesha anza kufanyiwa kazi ambapo ameogeza kuwa serikali imesha tenga kiasi cha shilingi milioni Arobaini zitakazotumika kununua mashine nyingine kwaajili ya kupampu maji yatakayo tumika katika kituo hicho.
Source(ITV)
Maoni
Chapisha Maoni