SIKU YA ALBINO DUNIANI KUADHIMISHWA ARUSHA JUNE 13 KITAIFA
WAKURUGENZI wa Halmashauri za wilaya nchini wameombwa kuwagharamia watu wenye ulemavu wa ngozi ili kwenda kushiriki maadhimisho ya siku ya albino kote duniani ambayo kitaifa yatafanyika juni 13 mkoani Arusha ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo juu ya siku ya watu wenye ulemavu wa ngozi, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi Kasim Kibwe amesema kuwa maadhimisho hayo yanakusudia kuongeza ufahamu juu ya ualbino kupitia mijadala, na kupata kauli za wadau ikiwemo Serikali ambapo kauli mbiu ni“DUMISHA AMANI NA ULINZI KATIKA JAMII KWA WATU WENYE UALBINO”.Source (Efm radio)
Maoni
Chapisha Maoni