UTAFITI UNAONYESHA KUWA NA UZITO MKUBWA KATIKA UMRI MDOGO KUNAWEZA KUSABABISHA UGONJWA WA SARATANI YA UTUMBO
SHIRIKA la kimataifa la utafiti wa Saratani limebaini kuwa binadamu kuwa na uzito mkubwa katika umri mdogo kunaweza kusababisha ugonjwa wa saratani ya utumbo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mtafiti wa masuala ya saratani kutoka shirika hilo la kimataifa RACHEL THOMSON zinasema kuwa uzito wa kupita kiasi unaweza kusababisha Kansa ya utumbo kwa kuwa kuna uhusiano wa karibu wa uzito mkubwa na ugonjwa huo.
Uchambuzi uliochapishwa kwenye jarida moja unaonyesha kuwa vijana wadogo wapo hatarini mara mbili zaidi kupata maradhi ya Saratani ya utumbo kutokana na kuwa na uzito uliozidi kiwango cha kawaida.Source(Efm radio)
Maoni
Chapisha Maoni