Dk Bilal amezindua chuo kikuu kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo akisistiza uwekezaji katika elimu ya sayansi kwa vijana.
Makamu wa rais Dk Mohamed Gharb Bilali amezindua chuo kikuu kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo mkoani Pwani akisistiza uwekezaji katika elimu ya sayansi kwa vijana kama hatua ya dira kusimamia vyema rasilimali za nchi ikiwemo madini, mafuta na gesi.
Makamu wa rais Dk. Gharibu Bilali katika kusistizaelimu ya sayansi amesema serikali itaendelea kufungua fulasa kwa watanzania na asasi mashirika ya dini ili kuwekeza katika elimu husisansa na tehama kama hatua ya kukidhi mahitaji na ushindani wa soko la ajira duniani na kuliepusha taifa kuendelea kutumia wataalam kutoka nje ya nchi.
Uzinduzi huo ulitanguliwa na ibada maalumu iliyongozwa na askofu kanisa katoliki mkuu jimbo la Morogoro Mhasham Telesphori Mkude ambaye katika kunukuu vitabu vitakatifu amewataka watanzania kujiepusha na watu wenye uchu wa madaraka pamoja na mafisadi wanaoweza kuliangamiza taifa hususan wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu octoba mwaka huu.
Awali makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT Padre Thadeus Mkamwa amsema chuo cha Marian ni chuo kikuu kishiriki cha SAUTI kilichochini ya shirika la kanisa katoliki na kwamba ni juhudi za kanisa hilo kuongeza udahii wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini sambamba na kutoa elimu ya sayansi ambayo ndio nguzo kubwa ya ulinzi wa rasilimali za nchin.
Source(ITV)
Maoni
Chapisha Maoni