Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa kutangaza rasmi kuwania urais kupitia CCM May 30.
Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa anataria kutangaza rasmi nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao tarehe 30 May jijini Arusha ambapo pia atatumia siku hiyo kujibu tuhuma mbalimbali zinazotolewa juu yake ikiwemo sakata la Richmond ambalo anadai ni njama zilizowekwa na baadhi ya wanasiasa kumchafua katika harakati zake za kisiasa.
Waziri mkuu huyo mstaafu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Monduli anaweka wazi msimamo wake huo katika mkutano maalum kati yake na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nyumbani kwake mjini Dodoma.
Katika mkutano huo ambao Mhe Lowassa alitoa fursa ya kuulizwa maswali ya papo kwa hapo na kuajibu licha ya kutumia muda mrefu kutoa ufafanuzi juu ya sakata la Richmond lakini pia amezungumzia baadhi ya vipaumbele vyake kama watanzania watamchagua kuongoza nchi ambapo lengo kuu atakaloanza nalo ni elimu kwanza akimani kuwa kila kitu kinategemea elimu.
Kuhusu matumizi makubwa ya fedha anayodaiwa kutumia katika safari yake ya kuwania urais Mhe Lowasa amesema fedha hizo anapokea kutoka kwa marafiki na hazina madhara yeyote katika harakati zake huku akidai kuwa hatalipa kisasi kwa lolote lililomtokea katika siasa na hana mpango wa kuondoka ndani ya CCM.
Source(ITV)
Maoni
Chapisha Maoni