Nigeria:Watu 29 wauawa msikitini
Watu 29 wameuawa katika mji wa Maiduguri
Watu 29 wameuawa kati mji mkuu wa jimbo la Borno Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria baada ya mlipuaji wa kujitoa mhanga kujilipua ndani ya msikiti.
Kamishna wa polisi katika jimbo la Borno amesema kuwa watu wengine 28 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.
Shambulizi hilo lilifuatia jaribio la awali la kuuteka ya mji wa Maiduguri lililondeshwa na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Wanagamabo hao walifyatua makombora kwenye makazi ya watu na kuua takriban watu 13.
Rais Buhari ameapa kukabiliana kikamilifu na wapiganaji wa Boko Haram
Siku ya ijumaa rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari aliahidi wakati wa kuapishwa kwake kuwa atakabiliana vilivyo na kundi hilo la wapiganaji wa Boko Haram.
Rais Buhari alisema kuwa kituo cha kijeshi kitawekwa katika mji wa Maiduguri kusadia kupigana na wanamgambo hao.
Rais Buhari akihutubia taifa punde baada ya kuapishwa alisema kuwa jeshi la taifa hilo litakita kambi yake katika mji huo wa Maiduguri ilikuitokomeza kabisa kundi hilo la waislamu la Boko Haram.
Wanajeshi wa Nigeria wakielekea Maiduguri
Awali Katika mahojiano maalumu na BBC, kiongozi huyo mstaafu wa jeshi amesema anatarajia kulishinda kundi hilo baada ya dhamira mpya kutoka jeshini na msaada wa nchi jirani.
"Kwa ushirikiano na majirani zetu Cameroon, Chad, Niger na jumuia ya kimataifa na dhamira ambayo tutapata kutoka katika jeshi, Nafikiri itachukua muda mfupi zaidi kukabiliana nao."
Jenerali Buhari amesema tayari ameainisha msingi wa tatizo linalokabili nchi ya Nigeria, lakini amewataka raia wa nchi hiyo kuwa wavumilivu.
"Tumebaini matatizo makubwa matatu.
Wanajeshi wa Nigeria waliwazidi maarifa wapiganaji wa Boko Haram
''Ambayo ni kukosekana kwa usalama nchini, tatizo ambalo kila mmoja analifahamu na lingine ni ukosefu wa ajira, hii ina maana uharibifu wa uchumi ikiwa ni kutokana na vitendo vya rushwa na rushwa yenyewe.
''Matatizo haya matatu makuu, Wanigeria wote wanafahamu na tunaomba ushirikiano wa wananchi wa Nigeria'',
''wasitarajie miujiza kutokea katika kuyapatia ufumbuzi matatizo haya katika kipindi cha miezi michache baada ya kutwaa madaraka kwa sababu uharibifu umechukua miaka mingi,
miaka kumi na sita ya utawala wa chama tawala cha nchi hii." Anasema rais huyo mpya wa Nigeria.
Source(Bbc Swahili)
Maoni
Chapisha Maoni