Burundi: rais asaini sheria juu ya kufadhili uchaguzi.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza aonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu kushindwa kwa jaribio la mapinduzi ya kijeshi.
Nchini Burundi, wakati ambapo wafadhili kadhaa wameamua kusitisha msaada wao kwa ajili ya mchakato wa uchaguzi, rais Pierre Nkurunziza amesaini sheria juu ya kufadhili uchaguzi katika nchi yake.
Sheria hii ya kirais inatoa ongezeko la nakisi na inapanga kupunguza bajeti za baadhi ya wizara kwa minajili ya kupatikana kwa euro milioni 25 sawa na bilioni 44 sarafu ya Burundi.
" Kutokana na uharaka na umuhimu wa kuiwezesha Tume Huru ya kitaifa ya Uchaguzi kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi ...", hayo ni maneno ambayo tunaweza kusoma kwenye sheria ya kirais yenye nambari 100/160, ya tarehe 21 Mei mwaka 2015, ambayo RFI imepata nakala. Sheria hiyo imetiliwa saini na rais Pierre Nkurunziza, makamu wake wa pili na Waziri wa Fedha.
Rais wa Burundi ameamuru shughuli mbalimbali ili pesa bilioni 44 sarafu ya Burundi ziweze kupatikana na hivyo kufadhili uchaguzi huo. Ili kupata kiwango hiki, kulingana na waraka huo, deni la ndani lazima " liwekwe kando ". Deni hili linakadiriwa kuwa sawa na bilioni 28 sarafu ya Burundi. Bilioni moja inatazamiwa kupatikana kupitia utaratibu mpya uliyowekwa ambao unajulikana kwa jina la " bidhaa nyingine " na bilioni 15 zitaondolewa kwenye taasisi nyingine. Miongoni mwa taasisi ambazo bajeti zao zitapunguzwa ni ofisi ya rais katika mradi wake unaojulikana kama "msaada kwa jitihada nzuri".
Si chini ya wizara tisa ambazo zitaathirika, ikiwa ni pamoja na wizara ya mambo ya Ndani, Sheria, Afya, Kilimo na wizara ya Elimu.
Upande wa wanadiplomasia kutoka nchi za Magharibi, hali hiyo inatia wasiwasi.
" Shirika la fedha dunia IMF na Benki ya Dunia vinaweza kujiondoa nchini Burundi kutokana na ongezeko la nakisi", amesema mmoja kati ya wanadiplomasia kutoka nchi za Magharibi, kabla ya kuongeza " viongozi wa Burundi wanataka uchaguzi ufanyike kwa hali na mali, bila kuzingatia athari ambazo zaweza kujitokeza baadae ".
" Afadhali kuwepo na mdororo wa kibajeti badala ya mgogoro wa kisiasa na usalama unaotokana na kutokuwepo na taasisi za uongozi wa nchi ", amejibu Willy Nyamitwe, mshauri mkuu wa rais Nkurunziza anayehusika na masuala ya mawasiliano.
"Ananaongeza ubaya juu ya ubaya"
" Nadhani ni kutoelewa majukumu yake, kwa rais anayemaliza muda wake na ambaye anasaini sheria ihusuyo bajeti ambayo inakakabiliwa na upungufu. Atachukua fedha kutoka wizara mbalimbali wakati ambapo wizara hizo hizo hazina pesa za kutosha na huenda wafanyakazi wakaanza mgomo", Jean Minani, kiongozi wa chama cha upinzani cha FRODEBU Nyakuri,
Source (RFI radio)
Maoni
Chapisha Maoni