Herieth Paul awa Mwanamitindo wa Mwaka kwenye tuzo kubwa za mitindo za Canada, CAFA

Mwanamitindo wa Tanzania, Herieth Paul ametwaa tuzo ya ‘Mwanamitindo wa Mwaka’ kwenye tuzo za sanaa na mitindo za Canada, CAFA.

Tuzo hizo ni maarufu nchini Canada na hutolewa kutambua watu wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya mitindo nchini Canada.
Herieth ambaye mwaka huu alichaguliwa kuwa mlimbwende msemaji wa brand maarufu ya urembo, Maybelline alihamia nchini Canada na familia yao na kuingia kwenye mitindo akiwa huko kabla ya kuhamia jijini New York.
Herieth Paul akiwa na supermodel Winnie Harlow.

Kupitia Instagram, supermodel wa Canada, Winnie Harlow aliandika: I had the honour of being apart of the CAFA Jury the same year @heriethpaul was nominated for Model Of The Year…. I think we know who I voted for. When your friends inspire you to be the best you can be, it’s meant to be! #ModelOfTheYear goes to the beautiful, sweethearted and talented HERIETH PAUL.”

Source:Bongo 5







































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..