Riek Machar aapishwa kuwa makamu wa rais Sudan Kusini..


Riek Machar
Aliyekuwa kiongozi wa waasi Riek Machar ameapishwa kuwa makamu wa rais wa kwanza nchini Sudan Kusini katika serikali mpya ya umoja.
Riek Machar ameapishwa mda mfupi baada ya kuwaasili katika mji mkuu wa Juba ,baada ya kuchelewa kwa kipindi cha juma moja hatua iliohatarisha kuanguka kwa makubaliano ya amani nchini humo.
Hiyo ni hatua muhimu ya makubaliano yanayolenga kumaliza mgogoro wa zaidi wa miaka miwili ambao umesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya raia huku takriban watu milioni mbili wakiwachwa bila makao.
Bwana Machar aliutoroka mji wa Juba wakati wa kuanza kwa mgogoro huo mnamo mwezi Disemba mwaka 2013.
Ametuhumiwa kwa kujaribu kupanga mapinduzi ambayo anakana ,lakini yalisababisha mauaji ya kulipiza kisasi ambayo yalipelekea kuwepo kwa mgogoro huo.
Kundi lake linasema kuwa kuchelewa huko kulisababishwa na mipango ya serikali na kwamba aikuwa amepanga kurudi siku ya Jumatano.
Taarifa kutoka kwa serikali siku ya Jumanne ilikuwa imesema kuwa kurejea kwa Machar kulicheleweshwa kwa kutaka kuwasili mjini Juba akiwa na silaha kali.




Source:BBC























































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..