Clinton, Trump wanatarajiwa kushinda New York..

Mdemocrat anayewania kugombea urais, Seneta Bernie Sanders akizungumza kwenye Communications Workers of America (CWA) huko Manhattan, New York.
Mdemocrat anayewania kugombea urais, Seneta Bernie Sanders akizungumza kwenye Communications Workers of America (CWA) huko Manhattan, New York.


Wajumbe wengi wanang’ang’aniwa katika jimbo la Kaskazini Mashariki mwa Marekani kwenye uchaguzi wa awali unaofanyika hivi leo. Kura za maoni zinamuoneyesha mgombea anayewania uteuzi kwa tiketi ya chama cha Demokratic Hillary Clinton na mgombea wa Republican, Donald Trump, wakiwa mbele ya wapinzani wao kwa kura nyingi.
Hakuna chama ambacho sheria zake zinaruhusu mgombea mmoja kuchukua wajumbe wote katika jimbo hilo, kwa hivyo hata yule atakayeshinda, kuna uwezekano kwamba wagombea wengine nao watazoa wajumbe wachache wa vyama vyao.
Seneta wa jimbo la Vermont, Bernie Sanders alielezea imani yake kwamba atashinda, licha ya uchunguzi wa maoni kumuonyesha akiwa pointi kumi nyuma ya Bi Hillary Clinton.
Sanders aliliambia shirika la habari la NBC kwamba katika siku za nyuma, aliwahi kumshinda Clinton kwenye maeneo ambayo uchunguzi wa maoni ulikuwa unamuonyesha akiwa ameshindwa na waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje.


Source:VOA




















































































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..