Viongozi wa mataifa 170 wakutana kutia saini mkataba juu ya hali ya hewa..
Viongozi wa takriban mataifa 170 wamekusanyika mjini New York, Marekani, ili kutia saini azimio la Paris, kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, miezi minne baada ya mkataba huo kujadiliwa na kupitishwa.
Maafisa wa umoja wa mataifa wanasema kwamba sherehe hiyo itakuwa ya kihistoria, kwani hakuna wakati mwingine katika historia, ambapo nchi nyingi hivyo, zimetia saini azimio kama hilo.
Hafla hiyo huenda ikaongeza kasi ya kutekelezwa kwa makubalianao hayo, ambayo utekelezaji wake ulitarajiwa kuwa umekamilika kufikia mwaka wa 2020, hata ingawa ni lazima mswada huo upitie taratibu za kisera katika nchi zinazotia saini. Marekani itawakilishwa na Waziri wa Mambo ya nje, John Kerry, kwenye sherehe hiyo.
Source:VOA
Maoni
Chapisha Maoni