Atolewa kwenye ndege kwa kuongea Kiarabu..
Mwanafunzi wa chuo kikuu raia wa Iraq katika jimbo la California nchini Marekani anasema kuwa alitolewa kutoka kwenye ndege ya shirika la ndege la Southwest baada ya kufanya mazungumzo kwa lugha ya kiarabu.
Shirika hilo la Southwest lilisema kuwa Khairuldeen Makhzoomi aliondolewa ndegeni tarehe 9 mwezi Aprili kabla ya ndege hiyo kupaa.
Bw Makhzoomi anasema alikuwa akizungumza na mjomba wake kwa njia ya simu kuhusu hotuba ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
Anasema kuwa mwanamke mmoja kwenye ndege hiyo alimkodolea macho wakati alitamka jina "Inshallah" akimaanisha Mungu akipenda.
Baada ya kutumia jina hili mfanyikazi wa shirika la Southwest alimsindikiza nje ya ndege.
Bw Makhzoomi ambaye aliingia nchini Marekani kama mkimbizi kutoka Iraq na sasa ni mwanafunzi wa chuo cha Carlifonia cha Berkeley, aliambiwa kuwa hawezi kuingia tena kwenye ndege hiyo.
Source:BBC
Maoni
Chapisha Maoni