Wabunge walalamikia kitendo cha kutorushwa Matangazo ya Bunge.
Baadhi ya wabunge wameonyesha kutoridhishwa na unataratibu mpya ya urushaji wa matangazo ya vipindi vya Bunge na kwa madai unalenga kuwanyima fursa wananchi kufahamu mwenendo mzima wa Bunge pamoja na utendaji wa wawakilishi waliowachagua katika kuwasilisha matatizo yao.
Wakizungumza kwa wakati tufauti baadhi ya wabunge wamedai mazingira ya kuzuia vyombo vya habari vya Television kurusha matangazo hayo mpaka kupitia kituo cha Bunge kuta kudumaza demokrasia na kuwanyima fursa wananchi kufahamu uwezo wa wawakilishi wao.
Aidha akielezea Changamoto hiyo inavyoathiri upinzani bungeni Mh .Msingwa amesema vyama vya upinzania vitaendelea kubadili mfumo wake kulingana na mazingira yaliyopo ili kukabiliana na hali hiyo kwa lengo la kuleta uelewa kwa jamii.
Aidha ITV imemtafuta waziri mwenye thamana ya habari,Mhe Nape Nnauye ili kutoa ufafanuzi wa changamoto zinazojitokeza kutokana na Bunge kuamua kurusha matangazo ya vipindi vya Bunge kwa kutumia studio zake ambapo ameahidi kukaa na wadau wa habari ili kuona namna ya kulitatua na kuweza kila mdau kutimiza wajibu wake bila ya kupata tabu.
Source:ITV
Maoni
Chapisha Maoni