Uhuru wa vyombo vya habari wapunguka Afrika...

Freedom House Press Freedom Report
Freedom House Press Freedom Report

Uhuru wa vyombo vya habari umekandamizwa zaidi Afrika na duniani kwa ujumla hapo mwaka 2015 kwa mujibu wa ripoti mpya ya taasisi ya kimarekani ya Freedom House.
Ukandamizaji mbaya zaidi huko Afrika umetokea Burundi ambako juhudi za rais kubaki madarakani baada ya muda mhula wake wa pili kumalizika umepelekea nchi hiyo kwenye ukingo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Katika nchi hiyo ya kanda ya maziwa makuu waandIshi wa habari wamefungwa, wamepigwa na kuuwawa na karibu vyombo vyote vya habari binafsi vimefungwa.
Freedom House inaeleza kwamba uhuru wa habari duniani ulishuka kufikia kiwango cha chini kuwahi kurikodiwa katika kipindi cha miaka 12.
Mataifa mawili ya Afrika yametajwa kua na hali mbaya kabisa kulingana na namna inavyovichukulia vyombo vya habari nazo ni Eritrea ambayo iko nafasi ya tano kwa ubaya na Equatorial Guinea iliyo nafasi ya nane kutoka nchi ya mwisho kwenye orodha ya Freedom House.


Source:VOA




























































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..