Julie Bishop: “Uingereza msijitoe katika jumia ya Ulaya”
Julie Bishop
Serikali ya Australia imewasihi watu wa Uingereza kutojitoa katika omoja wa Ulaya. Kura za maoni zitapigwa na Waingereza tarehe 23 mwezi wa sita mwaka huu.
Mapema mwezi huu Waziri wa mambo ya nje wa Australia, Julie Bishop, alifanya mazungumzo na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron katika mkutano wa usalama wa nyuklia ulifanyika Washington DC.
Bishop alisema anaamini kwamba ni kwa maslahi ya nchi yake Uingereza kubaki kuwa sehemu ya Umoja wa Ulaya.
Aliongeza kwa kusema Umoja wa Ulaya ni mshirika mkubwa wa biashara kwa Australia na kwamba Uingereza kuendeleza uanachama katika umoja huo wa nchi 28 ni muhimu.
Australia ambayo ni koloni la zamani la Uingereza na mahusiano yao ya kibiashara na kiuchumi yana historia ndefu. Upinzani ni mkali na waingereza wanaendelea kuhamia Australia kwa idadi kubwa wakati bunge la Canbera linafuata mfumo wa Westminster. Australia ina katiba ya ufalme huku Malkia Elizabeth wa Uingereza akiwa mkuu wake.
Bishop aliongeza kwa kusema, Umoja wa Ulaya ni chanzo kikubwa cha uwekezaji wa kigeni kwa Australia na ni mshirika wa pili kwa ukubwa kibiashara baada ya China.
Mashauriano ambayo hatimaye kuelekea kwenye mkataba huru wa biashara yanaendelea.
Ushirikiano wa biashara kati ya Austarlia na Uingeraza unafikia kiasi cha dola bilioni 16 kwa mwaka, wakati Uingereza ni ya tano kwa Uchumi duniani.
Wakati Bishop akiongela kuhusu Uchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili, baadhi ya wanasiasa wa Australia wanaisihi Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya kwasababu ya usalama wa taifa hilo pamoja na udhibiti wa mikapaka yake.
Seneta Mkonservative James Paterson aliliambia bunge la Australia kwamba wapiga kura wa Uingereza waachane na uanachama wa Umoja wa Ulaya.
Waziri mkuu David Cameron amewaomba viongozi wa dunia kuunga mkono mpango wake, wa Uingereza kubaki kwenye umoja wa Ulaya.
Naye rais wa Marekani Barack Obama alisema Uingereza itarudi nyuma kwenye makubaliano yao ya kibiashara na Marekani kama mahusiano yao na Umoja wa Ulaya yatavunjwa.
Source:VOA
Maoni
Chapisha Maoni