Ripoti ya CAG kuhusu UDA yazidi kulitikisa jiji la Dar es Salaam.
Siku chache baada ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za seriakli CAG, kutoa ripoti ya mwaka 2015, ikionyesha ukiukwaji wa sheria ya mauziano ya hisa za shirika la usafiri wa Dar es Salaam, UDA, uongozi wa jiji la Dar es Salaam umemuomba rais Dkt John Magufuli kuingilia kati sakata hilo ili mali hiyo muhimu kwa wakazi wa Dar es Salaam iweze kurejeshwa.
Katika mkutano na waandishi wa habari Meya wa Dar es Salaam Isaya Charles pamoja na masuala mengine katika bajeti yake ya jiji kwa mwaka 2016/17, wanatarajia kutumia zaidi ya bilioni 8 katika kutatua kero ya madawati, huku akiahidi kuhakikisha wanashirikiana na viongozi wengine ndani ya mkoa ili kuhakikisha wanaimarisha usafi wa jiji ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya utoleaji wa huduma za afya ndani ya jiji.
Kuhusu uuzwaji wa hisa UDA, jiji wanasema wanaungana na ripoti ya CAG, ambapo wamemuomba rais kuingilia kati sakata hilo, ilikunusuru mali ya umma iliyouzwa kinyume na sheria licha ya maafisa wa awali wa jiji kupuuza mapendekezo ya mwanasheria mkuu wa serikali na msajili wa hadhina waliopendekeza kutokuuzwa kwa rasilimali ya wana Dar es Salaam huku pia wakitilia shaka namna ukusanyaji wa mapato katika mradi wa DARTS.
Miongoni mwa mali zilizokuwa chini ya uongozi wa jiji na sasa kupelekwa kuwa chini ya mkoa wa Dar es Salaam ni jengo la machinga Complex lililogharimu zaidi ya bilioni 12, kwa ubia kati ya NSSF na jiji, ambapo sasa viongozi wa jiji wanasema hawatakuwa tayari kuona mali zao zikihamishwa na wao kuachiwa deni la zaidi ya bilioni 36.
Kwa mujibu wa jiji katika mwaka huu wa fedha 206/17 wanatarajia kujikita katika kusimamia, ukusanyaji wa mapato hasa kodi ya majengo, uimarishaji wa usafi ndani ya jiji, uboreshaji wa huduma za afya iki ni pamoja na kuhakikisha wanaziba mianya yote ya rushwa hasa kwenye miradi inayosimamiwa na halimashauri za jiji la Dar es Salaam.
Source:ITV
Maoni
Chapisha Maoni