Mkazi mmoja wa Arusha afikishwa mahakamani kwa kumkejeri Rais Magufuli kupitia mtandao wa kijamii.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA limemfikisha mahakamani mtu mmoja mkazi wa jiji la Arusha anayedaiwa kumkejeri Rais John Magufuli kupitia mtandao wa kijamii.
Akisoma shitaka ilo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Arusha Agustine Rusire mwendesha mashitaka wa Serikali Gaudensia Masanja amesema mshitakiwa Bw.Isaack Kabakuki alitenda kosa ilo March 17 mwaka huu eneo la Olasiti jijini Arusha huku akijuwa kuwa ni kosa na amekiuka sheria ya makosa ya mtandao kifungu cha 16 ya mwaka 2015.
Mtuhumiwa Bw.Isaack Kabakuki alikana kosa na kuomba apatiwe dhamana lakini upande wa mashitaka uliiomba mahakama isitoe dhamana kwakuwa upelelezi bado unaendelea pamoja na sababu za usalama wa mtuhumiwa japo mtuhumiwa alizikataa sababu hizo kuwa hazina msingi.
Source:ITV
Maoni
Chapisha Maoni