Hospitali ya Mkoa wa Singida yasema haitatoa rufaa kwa wagonjwa kwenda kutibiwa sehemu zingine kwakuwa ina madaktari bingwa wenye uwezo.
Hospitali ya Mkoa wa Singida haita toa rufaa ya wangonjwa kwenda kutibiwa katika Hospitali zarufaa kama Muhimbili,KCMC na Bugando mpaka hapo itakapo jiridhisha kwasababu mkoa una madaktari bingwa kumi na moja wa magonjwa mbalimbali ambao wanaweza kutoa huduma badala ya wagonjwa kufuata matibabu mbali.
Mganga mkuu wa mkoa wa Singida Dakatari.John Mombeki amesema hayo baada ya ya kufanya ziara ya kikazi katika Hospitali zote za mkoa wa Singida na kubaini kuwa mkoa una weza kutoa huduma kwa wagonjwa kwa kuwa kusanyanya madaktari bingwa mbalimbali ambao wata kuwa wakitoa huduma tembezi kwa kila wilaya kwa muda wa wiki moja na kupunguza kabisa wagonjwa kupewa wa rufaa kwenda nje ya mkoa.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya akina mama wa hospitali ya Mission ya Makiungu Sister Daktari Maria Borda ambaye ni daktari Mfawidhi wa Hospitali hiyo, amesema wanaishukuru Serikali kwa kuwa saidia badhi ya wahudumu wa afya,lakini pamoja na serekali kuwapatia fedha za uendeshaji changamoto kubwa ni fedha ya ruzuku kwa wafanyakazi ni ndogo kutoka serekalini.
Kwa upande wao wazazi na wagonjwa wanao patiwa huduma katika hospitali za makiungu,mtinko na St.Gasper Itigi ambazo ni za mashirika ya dini wameshukuru kwa kupatiwa huduma nzuri na wameiomba serekali kuendelea kuwapatia misaada kwa sababu imekuwa ikiwasaidia kuokoa maisha yao kutokana na sehemu zingine huduma za afya za serekali zipo mbali na wananchi.
Mkoa wa Singida una Hospitali tisa ,vituo vya afya kumina nane ,vituo vya kutolea huduma miambili na madaktari bingwa ambao wanfayankazi katika hospitali hizo kumina moja wa magonjwa mbalimbali.
Source:ITV
Maoni
Chapisha Maoni