Siku 5 baada ya Liverpool kumsimamisha Sakho, UEFA wamempa adhabu ya muda..
April 23, 2016 uongozi wa klabu ya Liverpool ulitangaza kumsimamisha beki wa kati wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea klabu hiyo Mamadou Sakho kutokana na kugundulika kutumia dawa za kusisimua misuli michezo, dawa ambazo ni kinyume na taratibu.
Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) leo limetangaza uamuzi au adhabu ya kumsimamisha Mamodou Sakho kwa siku 30, uamuzi ambao ni wa muda ili kuipa nafasi kamati ya maadili ya UEFA hadi itakapokaa na kutangaza adhabu rasmi.
Sakho ambaye alikuwa anachunguzwa na UEFA toka March 17 baada ya mchezo waEuropa league kati ya Man United dhidi ya Liverpool Old Trafford, amegundulika kutumia ‘Fat Burner’ kwa ajili ya kusisimua misuli, Mamadou Sakho atakumbana na adhabu kutoka UEFA baada ya kamati ya maadili kukaa na kuamua adhabu.
Source:Millardayo.com
Maoni
Chapisha Maoni