UMMY MWALIMU : MAPENZI YA JINSIA MOJA YANACHOCHEA KASI YA VVU

Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa Mkoa  wa Dar es Salaam pamoja na Dodoma imekuwa ikiongoza kwa vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Wizara ya Afya Maendeo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepiga marufuku matumizi ya vilainishi vinavyotumiwa na baadhi ya makundi yanayojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Akizungumza na  Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ni kinyume na sheria zilizoweka nchini na pia havitambuliki kabisa.

Amesisitiza kuwa serikali imeamua kuzuia vilainishi hivyo ambavyo vimekuwa vikitumiwa na baadhi ya makundi yanayojiusisha na mapenzi ya jinsia moja ili kupunguza ongezeko la maambukizi ya VVU.

“Kipaumbele cha serikali hii ni kujenga wodi za akinamama, kununulia vifaa vya kujifungulia pamoja na kununua madawa hospitalini na sio kutoa fedha kwa ajili ya vilainishi kwa makundi hayo” alisema Mwalimu.

Ameongeza kuwa makundi hayo yapo hatarini kwa kiasi kikubwa kupata maambukizi mapya ya VVU kutokana na kujihusisha na vitendo hivyo kwa kasi  zaidi.




Source:Mtembezi.com























































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..