Bilioni 1.6 kwa ajili ya uanzishwaji wa mfumo wa kielekroniki wa kusajili wakazi Tanzania..


Serikali imetenga Jumla ya shilingi bilioni 1.6 kupitia ofisi ya Taifa ya Takwimu na wafadhili wametoa shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya uanzishwaji wa mfumo wa kielekroniki wa kusajili wakazi Tanzania
 
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI Injinia Mussa Iyombe wakati wa kupokea maendeleo ya mfumo wa kuboresha upatikanaji wa taarifa sahihi katika serikali za mitaa.
 
Injinia Iyombe alisema mfumo huo unalenga kuwa na kanzi data ya watu wote nchini kiumri, uraia, jinsia, hali ya ulemavu, hali ya elimu, shughuli za kiuchumi, uhamaji na uhamiaji ikiwa ni pamoja ikiwa na vizazi na vifo.
 
“Taarifa hizi zitaisaidia serikali na wadau wengine kujibu maswali ambayo wengine tumekuwa tukijiuliza kila siku”.Alsema Injini Iyombe.
 
Alisema katika kutekeleza malengo Endelevu ya Maendeleo ya Mwaka 2030 serikali haina budi kuhakikisha wananchi wanaandikishwa katika rejesta ya wakazi ili iweze kuwafahamu mahitaji yake.
 
Aliongezea kuwa mfumo huo utasaidia upatikanaji wa idadi kamili ya wanafunzi waliopo mashuleni na kiasi gani cha fedha kinachotitajika kupelekwa shuleni, upatikanaji wa hali halisi ya uandikishaji wa watoto katika shule za msingi, mahudhurio shuleni na idadi ya walimu na taarifa nyingine.
 
Alisema kwa upande wa TAMISEMI mfumo huo utasaidia kuwagundua wazazi ambao hawana nia nzuri ya kuwapeleka watoto kuandikishwa kupitia katika kata zao kwa kutumia Global Positioning System za kaya zao katika ramani.
 
Akielezea faida za mfumo huo Injinia Iyombe alisema utaiwezesha serikali kufahamu idadi kamili ya watu wake kiumri na kijinsia kwa kuwa kazi hiyo itakuwa endelevu na itafanyiwa kazi kila siku na maafisa watendaji wa vijiji na mitaa kwa Tanzania nzima kwa kutumia teknolojia ya simu.
 
Aidha mfumo huo utaipa fursa Ofisi ya Takwimu ya kuwa na takwimu bora ambazo zitaipunguzia gharama ya kufanya tafiti za kila baada ya miaka mitatu, mitano hata kumi ikiwa ni pamoja na kupunguza maswali mengi ambayo huulizwa wakati wa sensa wa watu na makazi ambayo itafanyika tena hapa nchini mwaka 2022.




Source:Focusmedia.com



















































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..