KILICHOMKUTA ALIYETOA AMRI YA KUPINDUA SERIKALI UTURUKI..
Kanali Umit Gencer ambaye alitoa amri ya kusomwa na kutangaza kwamba serikali ya Ankara imepinduliwa katika jaribio la mapinduzi Julai 15 ametiwa mbaroni Uturuki.
Kanali huyo alitoa amri hiyo baada ya kufaulu kuingia katika jengo la kituo cha redio na runinga la taifa TRT.
Kanali Gencer alifikishwa mahakamani na kusomewa shitaka. Ifahamike kuwa Umit Gencer ni miongoni mwa wanajeshi walioasi na wenye ushirikiano na kundi la FETO ambalo linaongozwa na Fethullah Gullen ambaye ndio mchochezi mkuu wa jaribio hilo na kwa sasa yupo nchini Marekani
Wanajeshi wengine zaidi ya 300 wenye vyeo tofauti walikamatwa Jumamosi mjini Ankara kwa ajili ya uchunguzi.
Source:Mtembezi.com
Maoni
Chapisha Maoni