Chipanga: Mugabe ataongoza hadi kifo chake...

Mugabe
Mugabe ameongoza Zimbabwe tangu 1980
Kiongozi mmoja wa vijana katika chama tawala nchini Zimbabwe Zanu-PF amesema watu wasitarajie kwamba Rais Robert Mugabe, atastaafu.
Kiongozi huyo Kudzai Chipanga amesema Bw Mugabe, mwenye umri wa miaka 92 ataongoza kwa umri wake wote hadi atakapofariki.
Aidha, amesema: "Hata kwenye Biblia imeandikwa hivyo kwamba Mugabe, atawala hadi atakapofariki ''.
Ameyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wafuasi wa chama hicho wapatao 5,000 katika mkutano wa kisiasa mjini Harare.
Hatua hiyo ni kama majibu kwa upinzani nchini humo ambao umekuwa ukiendesha kampeni inayoonekana kuenea kupitia mitandao ya kijamii ikitumia kitambulisha mada #ThisFlag, maana yake Bendera Hii.
Kampeni hiyo imekuwa ikiendelezwa na kasisi mmoja aitwae Pastor Evan Mawarire:
Akiendelea kueleza kukasirishwa kwake na kampeni hiyo Chipanga ameongeza kusema: “Hamna kokote ilikoandikwa kuwa eti ‘Kasisi ataitawala Zimbabwe”.
Ameyataka maandamano hayo ya wapinzani yakome mara moja.
''Sisi hapa Zanu-PF, tulipambana na wakoloni hadi 1980 na tukawashinda, bado ndio tunatawala hapa na hamna kitakachobadilika,” akasema Bw Chipanga
Jana Robert Mugabe mwenyewe, ambaye amekuwa madarakani tangu 1980, alimshutumu Kasisi Evan Mawarire, ambaye amekuwa akimkosoa Rais Mugabe akimlaumu kwa kuporomoka kwa uchumi wa Zimbabwe na kumtaka ajiuzulu.
Mwezi jana Kasisi Mawarire, aliongoza mgomo mkubwa wa kumpinga Mugabe ambapo wafanyakazi waligoma kufika kazini siku hiyo.




Source:BBC



























































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..