YANGA SC YAENDELEA KUSHIKA MKIA BAADA YA KUKUBALI DROO YA 1-1 DHIDI YA MO BEJAIYA UWANJA WA TAIFA

Yanga imeshindwa kutamba kwa mara nyingine tena kwenye uwanja wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi yaMedeama SC ya Ghana katika mchezo wa Kundi A michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Donald Ngoma alianza kuifungia Yanga bao la kuongoza dakika ya pili ya mchezo huo akitumia vema makosa ya safu ya ulinzi ya Medeama na kuiweka timu yake mbele ya Medeama kwa bao 1-0..

Dakika 15 za kwanza watoto wa Jangwani walitawala mchezo kwa pasi za haraka huku wakiliandama lango la Medeama kitendo kilichosababisha wapate kona kadhaa..

Medeama walisawazisha bao hilo dakika ya 17 baada ya Bernard Dansokuunganisha mpira wa kona na kufanya matokeo kuwa 1-1 ambayo yalidumu hadi dakika 90 zinamalizika.

Mechi ya leo ilikuwa ni muhimu kwa vijana wa Hans van Pluijm kupata ushindi ambao ungewapa pointi tatu na kunyanyua morali ya kufanya vizuri kwenye kundi lao.

Yanga inaendelea kusalia katika nafasi ya mwisho kwenye kundi lake ikiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi tatu bila ushindi huku ikiwa imepoteza mechi mbili. Yanga ilifungwa goli 1-0 ugenini na MO Bejaiya ya Algeria kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi A kabla ya kukubali kichapo kingine kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo.

Medeama yenyewe inasalia kwenye nafasi yake ya pili kwa pointi zake mbili baada ya kucheza mechi tatu, ilifungwa 3-1 kwenye mechi ya kwanza dhidi TP Mazembe kisha ikatoka suluhu na MO Bejaia. Mazembe inaendelea kuongoza kundi hilo ikiwa na pointi sita mbele ya Bejaia yenye pointi nne kabla timu hizo hazijakutana zenyewe kwa zenyewe kwenye mchezo wa kesho.



Source:Lindi yetu.






















































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..