Marekani na Korea Kusini kuunda chombo cha ulinzi..

Generali Thomas Vandal, Mkuu wa vikosi vya Marekani huko Korea, na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Korea Kusini, Ryu Je-Seung
Generali Thomas Vandal, Mkuu wa vikosi vya Marekani huko Korea, na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Korea Kusini, Ryu Je-Seung



Marekani na Korea Kusini zimetangaza mipango ya kupeleka chombo cha ulinzi dhidi ya makombora kijulikanacho kama THAAD katika peninsula ya Korea ili kukabiliana na mpango wa nyuklia na makombora unaoendelea huko Korea Kaskazini.
Generali Thomas Vandal, mkuu wa vikosi vya Marekani huko Korea, na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Korea Kusini, Ryu Je-Seung, walitangaza ramsi mpango huo katika mkutano wa pamoja mjini Seoul mapema leo Ijumaa.
Hapo mwezi Februari kufuatia majaribio ya mwisho ya nyuklia ya Korea Kaskazini na kufyetuliwa kwa roketi ya masafa marefu kwa kutumia teknolojia ya makombora, Serikali za Washington na Seoul zilianza mashauriano rasmi juu ya uwezekano wa kupelekwa kwa THAAD.




Source:VOA






















































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..