Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2016

Anaswa na injini katika mashindano ya baiskeli..

Picha
Anaswa na injini katika mashindano ya baiskeli. Shirikisho la kudhibiti mashindano ya mbio za baiskeli, linachunguza iwapo mshiriki mmoja wa mbio hizo alitumia baiskeli yenye mota (Injini ndogo) katika mashindano. Chama cha UCI kimenasa baiskeli moja iliyotumika katika mbio za wanawake wenye chini ya umri wa miaka 23, katika mashindano ya uendeshaji baiskeli nchini Ubelgiji. Mwendeshaji baiskeli hiyo Femke Van den Driessche alikuwa amepigiwa upatu kuibuka mshindi wa mashindano hayo lakini akajiondoa kufuatia matatizo ya baiskeli. Bi Van den Driessche amekanusha madai dhidi yake anasema baiskeli hiyo inamilikiwa na rafiki yake. Bi Van den Driessche amekanusha madai dhidi yake anasema baiskeli hiyo inamilikiwa na rafiki yake. Rais wa Shirikisho la mashindano ya baiskeli- UCI, Brian Cookson anasema kuwa mshukiwa sio miongoni mwa washindi watatu wa kwanza katika mashindano hayo. Ikiwa udanganyifu huo utathibitishwa , itakuwa kisa cha kwanza kabisa kutambuliwa kama "ud

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda akamatwa..

Picha
Jenerali mstaafu David Sejusa amekamatwa majuma 3 kabla ya uchaguzi Mwanasiasa maarufu wa Uganda, Jenerali David Sejusa, amekamatwa, wiki tatu hivi kabla ya uchaguzi mkuu. Wakili wake amesema askari jeshi waliizunguka nyumba yake leo alfajiri. Inaarifiwa kuwa amewekwa katika kifungo cha nyumbani. Jenerali Sejusa alikuwa mshirika wa karibu wa Rais Yoweri Museveni, ambaye ameongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 30, anagombea uongozi tena katika uchaguzi wa tarehe 18 Februari. Jenerali Sejusa, alikimbilia nchi za nje miaka mitatu iliyopita, baada ya kumshutumu rais Museveni, kuwa alikuwa akimuanda kimyakimya mwanawe kurithi uongozi. Hii sio mara ya kwanza kwa mwanasiasa huyo kukamatwa, tangu kurudi Uganda. SOURCE:BBC

PICHA YA SIKU NA TASWIRA BLOG..

Picha
Edward Lowassa Na Waziri Mkuu Wa Tanzania Kassim Majaliwa.

Uzinduzi Wa Sherehe Za Miaka 39 Ya Kuzaliwa CCM Kisiwa Ndui Mjini Unguja.(+PICHAZ)

Picha
SOURCE:Michuzi Blog

Ugiriki:Wasusia mechi kupinga vifo vya wahamiaji

Picha
Ugiriki:Wasusia mechi kupinga vifo vya wahamiaji. Wachezaji wa timu mbili hasimu nchini Ugiriki wamesusia mechi wakipinga ongezeko la vifo vya wahamiaji wanaozama wakijaribu kuingia nchioni humo kukwepa vita Syria na Iraq. Wachezaji hao wa timu ya AEL Larissa na wenzao wa timu ya Acharnaikos waliketi chini pindi refarii alipopuliza kipenga cha kuanzwa kwa mechi hiyo ya ligi. Tukio hilo lililodumu kwa zaidi ya dakika mbili lilimwacha muamuzi asijue la kufanya! Hata ta hivyo alipoulizia cha mno akaelezewa kuwa muda mchache kabla ya mechi hiyo taarifa zilichipuka kuwa zaidi ya wahamiaji wengine 39 walikuwa wamekufa maji wakijaribu kuingia nchini humo wakitoroka vita. Taarifa hiyo iliwaudhi sana na kuwachochea kuchukua hatua hiyo. Wahamiaji hao walikuwa wametokea Uturuki wakijaribu kufika katika moja ya visiwa vya  Ugiriki lakini mawimbi makali yakaifanya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kuzama majini. Wahamiaji hao w