Wanzanzibari wametakiwa kuwa na subira wakati serikali ikitafuta suluhu ya mgogoro Zanzibar..



Watanzania leo wameingia mwaka mpya wa 2016 huku wito ukitolewa kwa wazanzibar kuwa na subira na uvumilivu wakati viongozi wa serikali kuu wa sasa na wale wa zamani wakitafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa uliopo visiwani Zanzibar.

Askofu mkuu msaidizi wa jimbo kuu katoliki la Dar es Salaam Titus Mdoe amesema hayo wakati akizungumza na ITV mara baada ya kumalizika  kwa ibada ya mkesha wa mwaka mpya wa 2016 katika kanisa kuu katoliki la mtakatifu Josefu.
 
Naye mchungaji kiongozi wa kanisa la Azania Front Charles Mzinga  amewataka watanzania kumkumbuka mwenyezi mungu kwa kutenda matendo mema kwani kuna wengi walitamani kufikia mwaka 2016 lakini waliishia njiani.
 
Waumini wa dini ya kikristo waliozungumza na ITV wamesema wameamua kuukaribisha mwaka mpya nyumba ya ibada kwa kuwa wanaamini kuwa bila uweza wa mwenyezi mungu wasingefika mwaka 2016.
 
Upande wa pili wa shilingi baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam walikuwa wakisherehekea kwa namba nyingine kuuona mwaka 2016. 







SOURCE:ITV















































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..