Wananchi wa Kimasai walalamikia kuporwa maeneo yao Siha mkoani Kilimanjaro.
Wananchi wa jamii wa Kimasia waishio katika kijiji Munge wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wamelalamikia halimashauri ya wilaya hiyo pamoja na chuo cha taaluma ya polisi Moshi kuwapora maeneo yao yenye ukubwa wa hekari 150 ambazo zilikuwa zinatumika kwa ajili ya kilimo na ufugaji.
Wananchi hao wanasema wanasikitishwa na hatua ya serikali ya wilaya kukaa kimya kwa zaidi ya mika kumi sasa tangu kuanza kwa mgogoro huo licha ya kufuatilia mara kwa mara bila mafanikio.
Wananchi hao wanaiombna serikali kuingilia kati mgogoro huo na kuupatia ufumbuzi ili kuwawezesha kuishi kwa amani kwa madai ya kuishi kama wakimbizi kwenye maeneo yao huku kijiji hicho kikiwa kinakabiliwa na ukosefu wa zahanati, maji masoko wala shule hali inayowalazimu wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda shule.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Donyomorwaq Bw.Iwite Ndossi anasema eneo hilo ni mali halali ya wananchi hao na kwamba wananchi hao wamekuwa wakitaabika kwa muda mrefu katika eneo hilo ambalo kwa sasa linatumiwa na chuo cha taaluma ya polisi Moshi kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi kwa vitendo.
Akizungumzia mgogoro huo mkurugenzi wa halimashauri ya wilaya ya Siha Bw.Rashidi Kitambulio amekiri kuwepo kwa mgogoro huo na kwamba tayari imeshatumwa timu ya kuchunguza mgogoro na kupima maeneo hayo na kwamba migogoro mingi katika wilaya hiyo inahusu mipaka.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni