ZEC yatangaza tarehe 20 machi kuwa siku ya marudio ya uchaguzi Zanzibar.



Hatimaye tume ya uchaguzi ya Zanzibar imetangaza tarehe machi 20 siku ya marudio ya uchagauzi mkuu wa Zanzibar ambao ulifutwa mwezi wa Oktoba mwaka jana.

Kauli hiyo ya marudio ya uchagzui  imetolewa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salim Jecha katika taarifa fupi iliyotolewa na ZEC kwa vyombo vya habari ambapo ITV imefanikiwa kupata taarifa hiyo ambapo amesema marudio hayo yametokana na uchaguzi wa awali kuwa na kasoro na tarehe hiyo imekubaliwa na tume yake.
 
Mara baada ya kutangazwa kwa tarehe hiyo wazanzibar ambao kwa muda mrefu wamekuwa na maoni na hoja mbalimbali za uchaguzi huo wametoa maoni yao ambapo kama iliyotarajiwa wengine wameunga mkono na wengine kuonekana kutokubali na kauli ya kuwepo marudia ya uchaguzi.
 
Kutangazwa kwa tarehe hiyo ya uchaguzi ni dalili za kuanza kwa harakati za kisiasa tena kisiwani Zanzibar ambazo zilisitishwa baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi na wananchi wakiendelea na shughuli zao kama kawaida.
 





SOURCE:ITV






















































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..