Mjumbe wa Rais Obama afanya mazungumzo na viongozi wa Burundi

Vijana wa kiume wakiwasalimia wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baada ya wajumbe kuwasili mjini  ‪Bujumbura
Vijana wa kiume wakiwasalimia wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa 

baada ya wajumbe kuwasili mjini ‪Bujumbura.


Burundi ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa tangu Aprili mwaka jana pale rais wa nchi hiyo alipotangazwa na chama chake kuwa atagombea urais kwa muhula wa tatu

Mjumbe maluum wa rais wa Marekani katika kanda ya Maziwa Makuu amemaliza ziara yake ya siku mbili  mjini  Bujumbura leo alhamisi .

Katika ziara hiyo ya Tom Perriero alikutana kwa mazungumzo na viongozi kadhaa wa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na rais wa Burundi,  Pierre Nkurunziza, makamu wake wa kwanza Gaston Sindimwo na spika wa Bunge la taifa ambaye pia ndiye mkuu wa chama tawala nchini humo Pascal Nyabenda.
Ziara hiyo ilikuwa ni kwa lengo la kuishinikiza serikali kukubali kukaa kwenye meza moja  na wapinzani wake ili kumaliza tofauti zao kwa amani. Hii ni baada ya mazungumzo chini ya usimamizi wa rais wa Uganda Yoweri Museveni yaliyozinduliwa mjini Entebbe  mwishoni mwa mwaka jana kukwama. 
Burundi ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa tangu Aprili mwaka jana pale rais wa nchi hiyo alipotangazwa na chama chake kuwa atagombea urais kwa muhula wa tatu.





SOURCE:VOA


































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..