Hatimae wakazi wa bonde la Mkwajuni wameanza kuondoka katika bonde hilo.
Hatimae wakazi wa bonde la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wamesalimu amri na kuamua kuondoka katika bonde hilo kufuatia mvua zilizoanza kunyesha na kuzidi kuharibu makazi yao ya muda ambayo awali yalibomolewa kwa lengoa la kuwataka waondoke mabondeni humo japo baadhi yao walikaidi agizo halali la serikali la kuwataka kuondoka.
ITV imefika bondeni hapo tofauti na siku mbili za nyuma idadi ya watu ambao walikuwepo katika eneo hilo ni ndogo sana huku idadi kubwa ya wanachi hao wakiwa wamekwisha fungasha vitu vyao na kuondoka wakiliacha bonde hilo tupu.
Katika hatua nyingine sehemu ya bonde hilo sasa limeanza kugeuzwa dampo na kutupa taka kutokana na kuwepo kwa idadai kubwa ya taka ambazo zinatupa hapo kila kukicha.
Baadhi ya wakazi wa jiji wamesema katika kipindi kama hiki ambacho tabiri zimeshatolewa kuhusu kunyesha kwa mvua serikali ijipange kuimarisha miundobinu yake ili kuondooa kero kwa raia wake.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni