Jeshi la Polisi lawashikilia watu 33 wanaosadikika kuwa ni waharifu mkoani Geita...



Jeshi la Polisi linawashikilia watu 33 wanaosadikika kuwa ni waharifu wamekamatwa mkoani Geita katika operationi maalumu ya kupunguza na hatimaye kutokomeza uhalifu mkoani Geita.

Miongoni mwa watuhumiwa hao wanne wamekamatwa kwa kosa la kukutwa na Bunduki moja ya kivita AK47 risasi 83 na bomu moja la kurushwa kwa mkono pia imekamata bunduki ya kienyeji aina ya Gobore, ambapo watu watano wamekamatwa kwa kosa la mauaji ya vikongwe na watu watatu walikamatwa kwa kosa la kuvunja na kuiba pia watu 17 walikamatwa wakipanga njama za kuiba katika mgodi mdogo wa Ibondo ambapo ilikamatwa kaboni  yenye thamani ya millioni miambili hamsini.
 
Aidha kamanda Mponjoli amesema vitu mbalimbali vimekamatwa katika operation hiyo ikiwemo Tv Rdio Computer na samani mbalimbali za ndani.
 
Kamanda Mponjoli amesema operation hiyo ni endelevu na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuhakikisha watu wanaishi kwa amani.






SOURCE:ITV





















































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..