Moto wateketeza majengo matano Darajani Zanzibar.



Moto mkubwa uliowaka kwa masaa manne huko darajani Zanzibar umeteketeza nyumba za familia tano na kusababsiha hasara ya mamilioni ya shilingi huku wananchi wakiendelea kuitaka serikali ikiimarishe kikosi cha zimamoto Zanzibar.

Moto huo mkubwa ulionza saa moja na  nusu usiku umeteketeza nyumba karibu tano zilizozunguka katika mtaa wa Darajani na kusababisha gharika kubwa zawakazi wa mtaa huo ambapo walilazimika kufanya kazi ya ziada ikiwa ni pamoja na kuwatoa watu wazima walikuwa wamo ndani ya nyumba hizo huku moto huo ukiwaka kwa kasi kubwa kutoka nyumba moja kwenda nyengine.
 
Pamoja na jitihada za kikosi cha zimamoto kufika eneo hilo bado askari hao walionekana kuzidiwa na kasi ya moto huo kutokana na ukosefu wa vitendea kazi vya kisasa na pia kukabiliwa na ukosefu wa maji katika magari yao na eneo hilo la Darjani, hali iliyosababisha wakazi wa eneo hilo kutumia maji ya majumbani na yale ya njiani kupambana na moto huo.
 
Uliweza kuthibitiwa ilipofika saa tano na nusu huku zoezi hilo likisimamiwa na mkuu wa kikosi hicho cha zimamoto Zanzibar ambaye aliweza kuhangaika kutoka sehmu moja hadi nyengine kuhakikisha moto huo unathibitiwa na kikosi chake ambapo akizungumza na ITV amesema maeneo ya Mjimkongwe yana changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maji na ufinyu wa bajeti.
 
Hata hivyo baadhi ya wananchi waliongea na ITV waliweza kutoa maoni yao ambapo wakaitaka serikali iwajenge mazingira mazuri ya kikosi hicho.
 
Hili ni tukio la kwanza kubwa la ajali ya moto kutokozea Zanzibar kwa mwaka huu ingawa nila nne kutokezea eneo hilo la Darajani katika kipindi cha miaka 2.









SOURCE:ITV














































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..