Afisa usalama feki akamatwa na vitambulisho vya chama cha mapinduzi mkoani Kilimanjaro...
Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamshilikilia Afisa usalama feki wa chama cha Mapinduzi ambaye amekamatwa katika ofisi za chama cha hicho katika kata ya kiusa jimbo la moshi mjini akiwa na vitambulisho vya watu tofauti tofauti akijifanya Afisa usalama kutoka ngazi ya taifa wa chama cha mapinduzi(CCM).
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Bw.Fulgence Ngonyani ametoa taarifa hiyo katika vyombo vya habari na kuwataka wananchi kuwa makini katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu ikiwa ni pamoja na kuwafichua watu ambao wanawatilia mashaka
Amesema mtu huyo ambaye amefahamika kwa jina la Ahmed Kimu ni mkazi wa uzunguni Dodoma na mkulima na kwamba jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi na hatimaye kumchukulia hatua za kisheria.
Nao baadhi ya vijana wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema katika kata ya Kiborloni wameliomba jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi katika kipindi hiki cha kuelekea kupiga kura Oktoba 25 kutokana na kuwepo kwa baadhi ya wagombea wa vyama vya siasa kupiga wafuasi wa vyama vingine.
Naye katibu wa Baraza la vijana wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema wilaya ya moshi mjini Deogratius Kiwelu amesema chama hicho kitahakikisha vijana wanajitokeza kupiga kura kwa utulivu bila vurugu ili kuhakikisha zoezi la uchaguzi linaisha kwa amani.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni