Msomi amtungia Nyerere kitabu.....



Hayati Mwalimu Julius Nyerere  Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Dar es Salaam.Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki Ruaha  Iringa, Profesa Gaundence Mpangala amemuenzi Mwalimu Julius Nyerere  kwa kuzindua  kitabu chenye  kurasa 16  kiitwacho, ‘’Historia ya Mkombozi  Mwalimu Julius Nyerere ‘’.
Kitabu hicho kimezinduliwa leo ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 16 ya  Kifo cha Baba wa Taifa,  kwenye ukumbi wa chuo kikuu cha Kikatoliki Ruaha Iringa .
Mpangala amesema; “Kitabu kina historia ya mwalimu tangu alipozaliwa mpaka kifo chake,hii inamaanisha kuwa kimeeleza maisha yake akiwa mtoto mpaka kukua,elimu yake ,alivyoingia kwenye siasa na maisha yake ya nyumbani.”
Amesema kitabu hicho pia kinaeleza maisha ya mwalimu akiwa rais ,akiwa rais mstaafu ,alivyopigania uhuru wa Tanganyika ,alivyokuwa mwadilifu,alivyopendwa na watu,alivyokuwa mshauri na kimbilio la wanyonge na mambo mengine mengi.
Mpangala amesema Mwalimu Nyerere alikuwa dira ya taifa na dunia nzima na alifanya mambo mengi ya kulikomboa taifa na kutatua migogoro ya Bara la Afrika.
Pia ameeleza kuwa ,watu wengi wamekuwa wakimuenzi mwalimu kwa maneno tu ambayo yanazungumzwa kisha yanaachwa.
“Namuenzi mwalimu Nyerere kwa maandishi ya vitu alivyovifanya, historia yake itakayo dumu hata kwa vizazi vijavyo na siyo kuishia kuzungumza tu kuwa mwalimu alifanya hivi na vile”amefafanua Profesa Mpangala.




SOURCE:Mwananchi






























   

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Imetangazwa noti yenye muonekano mzuri kuliko zote duniani kwa mwaka 2016..

Picha 10 za Ikulu zilizo nzuri zaidi Duniani...