Dr Magufuli amewataka watanzania kuendelea kudumisha muungano na amani ya nchi.



Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewahakikishia watanzania wote na jumuia za kimataifa kuwa uchaguzi mkuu utafanyika kwa uhuru, haki na kwa amani huku akionya wale wote hasa vijana wanaojaribu kuhatarisha amani ili kuuvuruga uchaguzi huo huku mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli akiwataka watanzania kuendelea kudumisha muungano na amani ya nchi.

Kabla ya kuelekea Pemba visiwani Zanzibara mgombea urais wa chama cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli amefanya mikutano ya hadhara katika maeneo ya Kisarawe mkoani Pwani na kisha jimbo la Ukongo jijini Dar es Salaam.
 
Mara baada ya mikutano hiyo Dr John Pombe Magufuli akiwa ndie waziri mwenye dhamana na ujenzi akashuhudia utiaji sahihi wa makubaliano ya ujenzi wa mradi wa barabara ya juu yaani fly over katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kipaumbele cha serikali ya awamu ya nne ilikuwa kuiunganisha mikoa yote kwa barabara za lami na sasa kipaumbele ni kupunguza msongamono wa magari katika majiji ya Tanzania.
 
Mara baada ya shughuli hiyo Dr John Pombe Magufuli akaelekea Pemba visiwani Zanzibar na kufa nya mkutano wa hadhara Pemba ambapo amewatahadharisha watanzania kuwa makini na wale aliowaita mamluki wanaounea wivu muungano wa Tanzania na Zanzibar.
 
Nae mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha mapinduzi Dr Mohamed Shein akawahakikishia watanzania na jumuia za kimataifa uchaguzi huru,haki na wa amani na kuwaonya wale wote wanaotaka kuleta chokochoko.







SOURCE:ITV

























Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Imetangazwa noti yenye muonekano mzuri kuliko zote duniani kwa mwaka 2016..

Picha 10 za Ikulu zilizo nzuri zaidi Duniani...