Wavuvi watakiwa kuhakikisha wanakuwa na vibali vinavyowaruhusu kuendesha shughuli hizo...



Tahadhari imetolewa kwa baadhi ya wavuvi wakubwa wa ndani na wa nje wanaoendesha shughuli za uvuvi katika baahari kuu ya Tanzania bila ya kibali kuhakikisha wanakuwa na vibali vinavyowaruhusu kuendesha shughuli hizo ikiwa ni pamoja na kulipa kodi inayostahili kwa serikali kwa kuwa serikali ijayo ya awamu ya tano chini ya Dr John Pombe Magufuli haitakubali eneo la bahari la Tanzania kugeuzwa shamba la bibi.

Tahadhari hiyo imetolewa na mgombea urais wa chama cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli wakati akizungumza na wananchi wa Kilwa Masoko mkoani Lindi na kuwaeleza kuwa serikali ijayo itahakikisha inaboresha shughuli za uvuvi  kwa wavuvi wadogowadgo ikiwa ni pamoja na kuwapatia mikopo ili waweze kuinuka kiuchumi na kuonya serikali yake haitavumilia shughuli za uvuvi haramu hasa unaoendeshwa na wavuvi wakubwa katika bahari kuu ya Tanzania huku 
serikali ikipoteza mapato.
 
Pia mgombea huyo wa urais wa CCM Dr John Pombe Magufuli amewataka watendaji wa serikali yake ya awamu ya tano kujipanga kuwatumikia wananchi hasa wa hali ya chini na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
 
Akitokea mkoani Lindi alikofanya mikutano ya kampeni takribani saba na kuingia mkoani Pwani safari iliyokuwa ikichelewa kwenda kwa wakati kutokana na mapenzi ya wananchi kwa Dr Magufuli kumsimamisha mara kwa mara barabarani ambapo baadhi ya wananchi wa wilaya ya Rufiji katika eneo la Kibiti wameelezea changamoto zinazowakabili huku wakimtaka Dr Magufuli atakapoingia madarakani kutekeleza ahadi iliyotolewa na Dr Jakaya Kikwete ya kujenga kwa lami barabara inayoelekea katika hospitali ya Mchukwi ili kuondoa changamoto ya usafiri kwa wagonjwa wanaokwenda kupata tiba katika hospitali hiyo.







SOURCE:ITV






















Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Imetangazwa noti yenye muonekano mzuri kuliko zote duniani kwa mwaka 2016..

Picha 10 za Ikulu zilizo nzuri zaidi Duniani...