Mgombea urais kupitia ACT Wazalendo ahidi kufufua mradi wa umeme wa upepo...
Mgombea urais kupitia chama cha ACT Wazalendo Anna Mghwira amekamilisha ziara yake ya kampeni katika mkoa wa Singida kwa kuahidi kufufua mradi wa kufua umeme kwa upepo ili kumaliza tatizo la umeme katika mkoani huo na mikoa jirani.
Akihutubia mikutano tofauti katika vijiji vya Makiungu, Dung’unyi, Ikungi na Singida mjini, Anna Mghwira ambaye anatumia kauli mbiu ya utu, uadilifu na uzalendo amesema upepo mkali uliopo katika mkoa huo kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa unaweza kuzalisha umeme na hivyo kupunguza tatizo la umeme nchini.
Katika hatua nyingine akiwa mjini Singida amemtaka rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete na tume ya taifa ya uchaguzi kuitisha kikao cha wenyeviti wa vyama ili kujadili changamoto hasa wakati wa upigaji kura na kwamba suala la kukaa mita mia mbili baada ya kupiga kura ni la kisheria na sio matakwa ya mtu.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni