NEC yavionya vyama vya siasa kuacha kutoa taarifa za uongo kwa wafuasi wao...



Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) imevionya vyama vya siasa kuacha kutoa taarifa za uongo kwa wafuasi wao dhidi ya tume hiyo na badala yake watoe taarifa sahihi kuhusu tume na kujikita kuwaelimisha wafuasi wao na wananchi kujitokeza kupiga kura Oktoba 25 mwaka huu.

Onyo hilo limetolewa na kamishna wa tume hiyo Bi. Mary Longway wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa na watendaji wa tume hiyo mjini Songea mkoani Ruvuma.
 
Kamishna huyo amesema kama vyama vya siasa vitawahamasisha wafuasi wao kubaki kwenye vituo vya kupigia kura kutakuwa na uwezekano wa kutokea vurugu zitakazowatisha wapiga kura kujitokeza kupiga kura huku kaimu mwenyekiti wa Chadema mkoani Ruvuma Bw. Rashid Chitepete akisema ni lazima wawe jirani na vituo vya kupigia kura ili kuwepo na watu wa kuwatangazia matokeo.
 
Naye kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma ACP Mihayo Msikhela amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuhubiri amani  kwa wafuasi wao.









SOURCE:ITV















Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Imetangazwa noti yenye muonekano mzuri kuliko zote duniani kwa mwaka 2016..

Picha 10 za Ikulu zilizo nzuri zaidi Duniani...