Christiano Ronaldo Afikisha Goli La 324 Baada Ya Ushindi Wa Real Madrid Dhidi Ya Levante..

CRISTIANO RONALDO


CRISTIANO RONALDO Leo amefunga Bao 1 na kukamata Rekodi ya Real Madrid ya kuwa Mfungaji Bora katika Historia yao akiwa na Bao 324 akimpiku Raul.

Leo, Uwanjani Santiago Bernabeu, Real iliichapa Levante Bao 3-0 na kukwea kileleni mwa La Liga.


Bao za Real zilipachikwa na Marcelo katika Kipindi cha Kwanza na Ronaldo na Jese kupiga Bao nyingine katika Kipindi cha Pili.

Real wamekamata usukani pengine hadi kesho ikiwa waliokuwa Vinara Villareal watashinda Mechi yao na Celta Vigo.
CRISTIANO RONALDO


RATIBA LA LIGA (Saa za Bongo)
Jumapili Oktoba 18
1300 Villarreal v Celta Vigo
1700 Real Sociedad v Atletico Madrid
1915 Getafe v Las Palmas
2130 Deportivo v Athletic Bilbao

Jumatatu Oktoba 19
2130 Sporting Gijon v Granada










SOURCE:Lindi Yetu





















Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Imetangazwa noti yenye muonekano mzuri kuliko zote duniani kwa mwaka 2016..

Picha 10 za Ikulu zilizo nzuri zaidi Duniani...