Tunduma yashindwa kuhimili kishindo cha Lowassa...




Mji wa kibiashara wa Tunduma umejikuta ukisimamisha pilika pilika zake zote za kibiashara kupisha mkutano mkubwa na wa aina yake uliokuwa ukiongozwa na mgombea urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa aktiba ya wananchi UKAWA,Edward Lowassa.

Wanasema si rahisi kuwasimamisha wafanya biashara mjini Tunduma, lakini Oct 17, walisalimu amri na kuweka chini biashara zao.
 
Mara kwa mara maelfu hawa walikuwa wakishindwa kuzuia mahaba yao kwa mgombea huyo wa nafasi ya urais Edward Lowassa.
 
Hata hivyo mkutano huu unaotajwa kuvunja rekodi mjini Tunduma uliingiwa na hitilafu ya mitambo ya sauti ambapo licha ya juhudi nyingi tu za kubadili vifaa ilishindikana na Freeman Mbowe akazungumza na wanatunduma na kuaahidi kurejea Tunduma hapo kesho Oct 18.
 
Lakini kwa wakazi wa tunduma wanasema inyeshe leo inyeshe kesho bado wanaimani na Edward Lowasa.
 










SOURCE:ITV






















Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Imetangazwa noti yenye muonekano mzuri kuliko zote duniani kwa mwaka 2016..

Picha 10 za Ikulu zilizo nzuri zaidi Duniani...