Wachezaji 5 Bora Wa Mda Wote Afrika Wanaocheza Mpira Wa Kikapu (Basketball) NBA...(+PICHAZ)
National Basketball Asssociation (NBA) ni ligi ya mpira wa kikapu unaochezwa na wanaume Amerika ya Kaskazini, unaweza kusema inaegemea sana Amerika. Huwa wanatembelea Dunia nzima kutafuta wachezaji wenye vipaji na wanaoujua mpira huo wakikapu.
Na asili ya wachezaji wengi wa NBA ni kutoka Afrika, na tunaweza kusema shukrani nyingi kwa NBA kwa kuifanya Nchi nyingi za Afrika kwasasa kuwa na Mchezo huo wa kikapu na kufanya mashindano yawe magumu na yenye upinzani mkubwa kati ya Timu na Timu.
Lakini leo tunavyouzungumzia Mchezo huo kwa Mastaa wa Mpira wa kikapu kutoka Nchi za Afrika wameendelea kuimalika zaidi katika michezo yao wanayocheza..
Na hawa ndio Mastaa bora Watano Kutoka nchi za Afrika wa wakati wote katika mchezo huo wa Kikapu.....
1. BISMACK BIYOMBO
Alizaliwa Agosti 28,1992, Bismack Biyombo ametokea nchi ya kidemokrasia ya Kongo, na kwa mara ya kwanza alichukuliwa na timu ya Scramento Kings 2011. Baada ya kutoka Scramento Kings alichukuliwa na Timu ya Charlotte Bobcats tarehe 19 Desemba mwaka huo huo. Na yupo katika orodha ya wacheaji kutoka Afrika wanaolipwa mshahara mkubwa.
2. LUOL DEN
Alizaliwa tarehe 16, April 1985 Wau, Sudani ambayo kwasasa inaitwa Sudani ya Kusini, Luol alikulia katika nchi ya Uingereza alipokwenda kujiunga na High School, Blair Academy ya Blairstown, New Jersey. Alikuwa mchezaji wa Chicago Bulls kutoka mwaka 2004 mpaka 2014.
3. HAKEEM OLAJUWON
Hakeem Olajuwon alizaliwa Lagos, Nigeria, mwaka 1963. Amecheza NBA kwa miaka 18. Hakeem hakuwahi kucheza mpira wa kikapu mapaka pale alipokwenda Marekani ndipo akaanza kuucheza mchezo huo na alikuwa ni bora zaidi katika nafasi ya katikati. Na ameshinda ubingwa wa NBA KWA mara mbili.
4. HASHEEM THABEET
Hasheem amezaliwa tarehe 16 Februari, 1987, katokea Jiji la Dar es salaam, nchini Tanzania, kwasasa anachezea katika timu ya Oklahoma City.Alianza kucheza mpira wa kikapu akiwa na umri wa miaka 15. Na pia ni mmoja wa wachezaji wakikapu kutoka Afrika anayelipwa mshahara mkubwa.
5.STEVE NASH
Amezaliwa tarehe 7 Februari 1974, Jijini Johannesburg, Afrika ya Kusini, amekulia katika nchi za Uingereza, Columbia na Canada. Steve anacheza kama mchezaji wakupata point zaidi na amemaliza NBA kwa misimu 15, akiwa amefunga kwa wastani wa point 14.6 kwa kila mechi, na kwa kutoa assist kwa kila mechi ni wastani wa 8.5.
:Imeendaliwa na Geofrey Eston (Taswira Blogger) kwa msaada wa Tovuti ya AnswersAfrica.






Maoni
Chapisha Maoni