Bodi ya rushwa ya AU yaridhishwa na serikali ya Tanzania katika kudhibiti rushwa...
Wajumbe wa bodi ya kupambana na rushwa kwa nchi za umoja wa Afrika (AU) wameelezea kuridhishwa kwake na misingi iliyowekwa na serikali ya Tanzania ya kudhibiti vitendo vya rushwa haswa wakati huu wa uchaguzi.
Wakizungumza baada ya kumaliza kikao chao cha kutathmini hatua iliyofikiwa kukabiliana na rushwa kwa nchi za umoja wa Afrika mwenyekitia wa bodi hiyo Daniel Batdam amesema pamoja na changamnoto zilizopo hatua iliyofikiwa na Tanzania katika kukabiliana na rushwa inafaa kuigwa na nchi zingine.
Aidha Bw.Batdam ameitaka Tanzania kuendelea kuziba mianya yote ya rushwa wakati huu wa uchaguzi ili uchaguzi uweze kumalizika kwa amani na kuendelea kuwa mfano wa nchi za umoja wa Afrika zenye hazina kubwa ya amani.
Wajumbe wa bodi hiyo ambao wamekutana jijini Arusha kwa siku tano pia wamejadili masuala mbalimbali ya miradi ya maendeleo ukiwemo wa uenzi wa makao yake makuu yanayojengwa hapa nchini katika mkoa wa Arusha.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni