Kaburi la halaiki lapatikana Burundi..
Utawala wa mji mkuu wa Bujumbura Burundi wamegundua kaburi la halaiki linaloshukiwa kuwa na takriban miili 30. Maafisa wa polisi na utawala wa mji mkuu wa Bujumbura Burundi wamegundua kaburi la halaiki linaloshukiwa kuwa na takriban miili 30. Mwandishi wa BBC aliyeko huko Prime Ndikumagenge anasema kuwa miili 3 na fuvu la kichwa ilipatikana katika eneo la Mutakura Kaskazini mwa Bujumbura. Kitongoji hicho cha Mutakura ni moja ya ile iliyosheheni wafuasi wa upinzani ambao walijitokeza mabarabarani wakiandamana kupinga kauli ya rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu uongozini. Nkurunziza alitangaza nia ya kuwania muhula wa tatu mwezi Aprili mwaka uliopita kinyume cha katiba akidai kuwa mhula wa kwanza hakuchaguliwa na umma. Meya huyo leo amekiri kuwa utawala wake ulizika miili ya watu 58 katika makaburi ya halaiki katika makaburi yanayofahamika. Wapinzani wake hata hivyo wanadai kuwa alikiuka katiba ya taifa. Meya wa mji wa Bujumbura Freddy Mbonimpa anasema wa...